Lulu Diva Adai Anamiliki Gari La Thamani Kuliko Wasanii Wote Tanzania

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Ona’ amekiri kuwa yeye ndio msanii anayemiliki gari la thamani Tanzania nzima.

Lilu Diva amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv, ambapo Lulu Diva aliulizwa kuhusu mali zake na kuulizwa kama ana mpango wa kubadilisha gari anayotumia.

download latest music    

Lulu Diva alifunguka na kusema hana mpango wa kubadilisha gari kwa sababu gari lake ni zuri na la thamani kuliko magari yote ya wasanii hapa Bongo:’

Hapana sina mpango wa kubadilisha gari lakini nitabadiisha rangi kwa sababu sijaona gari ambayo ninaweza nikabadilisha tofauti na Jeep naipenda sana”.

Halafu pia katika wasanii wote mimi peke yangu ndio nina gari nzuri halafu la thamani nyie wenyewe mkiangalia mnaona na sio kitu ambacho naongea ili kujisifia ila am proud of myself”.

Lulu Diva amesema hajanunuliwa na mwanaume hilo gari bali ni kwa juhudi zake mwenyewe amenunua gari pamoja na nyumba kutokana na biashara zake na ukulima wa kahawa anaofanya.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.