Lulu Diva Adaiwa Kulitema Penzi la Mwanaume Anayemuweka Mjini Kisa Rich Mavoko

Mwanamuziki wa Bongo fleva Lulu Diva amedaiwa kulitema penzi la mwanaume aliyekuwa anamuweka mjini ‘Sponsa’ kisa na mkasa ni penzi la mwanamuziki mwenzake kutoka WCB Rich Mavoko.

Mambo yanasemekana sio mambo kwani Lulu Diva anadaiwa kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu ambaye ndiye aliyekuwa anamuweka mjini msanii huyo mrembo au wenyewe wadada wa mini wanawaita ‘Sponsa’.

download latest music    

Tetesi za Lulu diva kuwa na uhusiano na mkali wa Bongo fleva Rich Mavoko zilanza kuenea kitambo kirefu kweli ingawa inajulikana wazi kuwa Lulu Diva ana mpenzi wake mwingine ambaye mwenyewe amekiri kumpenda.

Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwa na habari za Lulu Diva kuolewa na mwanaume huyo ambaye habari za chini ya kapeti zinasema mwanaume huyo anaishi nchini South Africa lakini ndiye anaye mwezesha Lulu Diva yaani anamuweka mjini.

Inhawa mwenyewe Lulu mara kwa mara amesisitiza kuwa hana uhusiano wowote na mavoko zaidi ya kazi za kisanaa lakini picha zao zilisambaa mtandaoni miezi michache iliyopita zilisema vinginevyo kwani walikuwa wamekaa mikao ya kimahaba sana.

Pia chanzo cha habari hii kilidai kuwa picha zile zilizowaonyesha Luludiva wakiwa pamoja club pia zilimkasirisha mpenzi huyo wa Lulu diva hali iliyompelekea kumpiga kibuti lakini kwa sasa penzi la Lulu Diva na Mavoko linasemekana kuwa moto moto.

Baada ya habari hizi za kimbea kusambaa gazeti la GPL lilijaribu kumtafuta Lulu diva lakini baada tu ya kusikia alichoulizwa alikatiwa Simu lakini pia baada ya Mavoko kutafutwa alisema hawezi kuongea chochote kwani hajaruhusiwa kusema chochote na uongozi wake wa WCB.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.