Lulu Diva aeleza kwanini mwanaume atakaye muoa atatoa idadi ya ngombe anazotaka yeye

Lulu Diva amesema kuwa yeye ndo ataambia mwanaume atakaye muoa idadi ya ngombe anazopaswa kutoa. Muimbaji huyo alisema hadhani kuwa kuna mwanaume yeyote ambaye anaweza kataa kutoa ngombe anazotaka yeye.

Mrembo huyo anadai kuwa uzuru wake ndo chanzo cha yeye kupewa kitu chochote anachotaka na wanaume. Akiongea kwa kipindi cha Uhondo cha E FM, Lulu Diva alieleza kuwa yeye ni mrembo kutokana na sifa alizokuwa akipewa na mama yake mzazi.

download latest music    
Lulu Diva

“Mimi ni msichana ambaye nipo sex ambaye nina mvuto, mama yangu alikuwa akiniambia Lulu mwanangu mashallah, yaani hapa sidhani kama kuna mtu nitamwambia idadi ya ng’ombe ninazozitaka halafu akapindua. Na mimi mwenyewe nikawa najiona ndio maana hata sikuweza kurubunika, yaani ile mtu kuniambia wewe mzuri akanidanganya kwa vichipsi mayai, mwenyewe nilishajijua ni mzuri,” amesema Lulu Diva.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere