Lulu Diva aeleza ukweli kuhusu madai kuwa anashiriki mapenzi na Jaguar

Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva anadaiwa kushiriki mapenzi na msanii Jaguar kutoke nchi jirani ya Kenya.

Jaguar ni meneja wa mrembo huyo kutoka Tanzania lakini kuna wale wanaodai kuwa wasanii hao wawili wanashiriki mapenzi chini ya maji.

download latest music    
Jaguar

Lulu Diva hata hivyo aliambia Star Mix kuwa wambeya wametunga tu hadhiti kuwa yeye na Jaguar ni wapenzi ilhali wao wanahusiana tu kikazi.

“Ni uzushi kama unavyojua Wabongo, Jaguar ni meneja wangu tu ambaye ananisaidia katika kunisimamia katika muziki na si vinginevyo,” Lulu Diva aliambia Star Mix.

Lulu Diva

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere