Lulu Diva Akanusha Kuwa sababu ya Ugomvi wa Diamond na Rich

Mwanadada Lulu diva amefunguka alipokuwa akiongea na bongo 5 na kukanusha taarifa kuwa kumekuwa na ugoimvi kati ya rich mavoko na Diamond Platinumz na kusababisha Rich Mavoko kushindwa kuendelea kufanya kazi na WCB.

Lulu diva anasema kuwa pamoja na hayo yote , hajui kama kuna ugomvi kati ya Diamond na Rich ila kama wameshindwa tu kufanya kazi pamoja , lakini hata hivyo anasema kuwa yeye na Diamond wamekuwa wakiheshimiana sana kiasi kwamba hawawezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi.

download latest music    

Lulu Diva amekanusha kabisa tetesi hizo kuwa aliwahi kuwa na mahusiano ya siri na bosi wa Rich na kusababisha Rich kuondoka  baada ya siri hiyo kuvuja na kisha kusema kwa anavyojua yeye hakuna ugomvi katI ya wawili hao.

Nyinyi waandishi ni waongo, sijawahi  na haiwezi kutokea na pia mimi na Diamond hatujawahi kuwa na mahusiano na mimi ninamuheshimu sana Diamond na wala sidhani kama kuna ugomvi kati ya  Rich na Diamond kabisa.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.