Lulu Diva Akiri Kulaumiwa Sana Kwa Kuiba Madanga Ya Watu

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Ona’ amekiri kuwa wanawake wengi wamekuwa wakimlaumu kwa kuiba wanaume wao (madanga).

Lulu  Diva amekiri kwamba ameshakutana na tuhuma nyingi kutoka kwa wanawake kadhaa ambao wamekuwa wakimtuhumu kwa kuwachukulia wanaume zao.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Kipindi cha ‘Now you Know’ Lulu Diva amefungukia tuhuma hizo na kusema haya:

Nimeshakutana na hizo kesi sana unakutana na mtu anasema “Unatembea na bwana angu umemchukua” sasa mimi najiuliza mwanaume anachukuliwaje? Anachukuliwa au anakuja mwenyewe”.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa Lulu Diva Anatembea na mwanaume mwenye pesa Chafu na hata ilisemekana kuwa mwanaume huyo ni Kigogo wa serikalini tetesi ambazo mwenyewe amezikataa mara kwa mara.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.