Lulu Diva Anyang’anywa Mali Zote , ni Baada ya Kurudisha Mahari.

Siku kadhaa nyuma zilizopita Lulu Diva alikiri kurudisha mahari kwa mwanaume aliyetaka kumuoa huku akisema kuwa mwanaume huyo alikuwa akifata sana na kusikiliza maneno kutoka kwa ndugu zake ambao walikuwa hawataki yeye kuolewa katika familia hiyo, huku maneno  ya chinichini yakisema kuwa Lulu Diva alishindwa kuolewa kwa sababu mwanaume huyo aligundua kuwa Lulu Diva anatoka kimapenzi na msanii mweznie ambae ni Rich Mavoko.

Akifahamika kwa jina moja la Joho, mwanaume huyo ndie inaesemekana kuwa alikuwa akimpa lulu diva kila kitu alichokuwa akionekana kuwa nacho kama nyumba, gari na ela za kila siku lakini mwanaume huyo aliamua kubadilisha mawazo na kumpokonya kila kitu baada ya kuoa kuwa Lulu Diva hataki kuendeleza na kuheshimu mahusiano yao.

download latest music    

Lulu Diva ambae alikuwa akionekana na vitu hivyo , alipewa na mwanaume huyo ambae alikuwa akiishi  na kinyumba kwa zaidi ya miaka mitatu lakini wameshindwana na ameamua kuchukua vitu vyako.

Hata hivyo Lulu mwenyewe amekuwa akijitapa kuwa vitu hivyo vya thamani amepewa na kigogo mmoja wapo Tanzania.Akiongea na GPL, moja ya watu wa karibu wa Joho aliongea na kutoa siri ya lulu diva kwa kumuona muongo na kujitangazia kitu kisichokuwepo.

hivi unajua huyo lulu ni muongo sana,mbona gari analosema amepewa na kigogo  alipewa na rafiki yangu  joho na walikuwa wakiihsi nyumba moja  ila sasa wameachana na ninavyojua ni kwamba ameshalichukua gari lake.Hiyo yote ni baada ya kumshutukia kuwa lulu diva anatembea na msanii mwenzie rich mavoko.

Baada ya tetesi hizo kusambaa, GPL iliamua kumtafuta msanii huyo na kumuuliza kuhusu ukweli wa tetesi hizo ambapo Lulu Diva alikiri kununuliwa gari na joho lakini sio hilo alilonalo sasa hivi.

Yaani sitaki kukumbuka maana kipindi niko na joho alinitenda sana kiasi kwamba nilikuwa nikikesha nalia kila siku , alinifukuza kwenye nyumba nilikuwa ninakaa na hata  gari aliloninunulia alinipokonya ambapo kwa mtu yoyote lazima alifananishe kwa sababu ya rangi lakini ile ilikuwa BMW, na hii ni Jeep.

Lulu diva akiwa katika pozi na magari tofauti tofauti ya kifahari.

 

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.