Lulu Diva Ataja Kinachomkondesha Mavoko Baada Ya Kuondoka WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva mwanadada Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka na kusema kinachomkondesha Rich Mavoko hivi sasa ni mazoezi na sio stress za WCB.

Mwezi uliopita Msanii Rich Mavoko ambaye alikuwa WCB kwa miaka kadhaa alitangaza kuondoka katika Label hiyo Rasmi na sasa anajitegemea mwenyewe na Label yake ya Bilionea Kid.

download latest music    

Lakini tangu ameanza kufanya Muziki wake mwenyewe Kumekuwa na taarifa kwamba Mavoko amepungua mwili kwa kasi na maneno kusemwa kuwa kuondoka WCB imekuwa tatizo kwake.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari Lulu Diva ambaye anatajwa kuwa ni mpenzi wa Mavoko amefunguka na kusema sio kweli taarifa za Mavoko kukondeshwa na WCB bali ni mazoezi anayefanya:

Rich anafanya mazoezi Tena makali sana, mimi mwenyewe huwa natamani kufanya mazoezi yake lakini siwezi naishia kusema kesho kesho.

Sio kweli amekonda kwa sababu ameondoka WCB kwa sababu ameondoka mwenyewe angekuwa amefukuzwa ingekuwa bora zaidi”.

Baada ya kuondoka WCB, Mavoko ameachia ngoma yake inayoitwa ‘Ndegele’ ambayo inafanya vizuri sana na ipo namba Tatu Kwenye trending Youtube.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.