Lulu Kutumikia Kifungo Chake Cha Nje Kwa Kufanya Usafi Wizarani

Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu alipata msamaha wa Raisi na kupunguziwa adhabu ya kifungo chake na hivyo kutoka gererzani na kutumikia nje.

Jeshi la Magereza lilitangaza taarifa hiyo kwa vyombo vya habari baada ya kumuachia mfungwa huyo ambaye alikuwa anatumikia kifungo chake Segerea baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba.

download latest music    

Akiwa nje, Lulu amepangiwa kufanya kazi mbali mbali za kijamii ikiwemo katika viunga vya wizara ya ndani ya nchi, kwa mujibu wa amri ya mahakama  kuu.

Inadaiwa kuwa Lulu akiwa na wenzake 10 wamepangiwa kufanya usafi katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani zilizopo Posta Jiji la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka  Mkurugenzi wa Probesheni na Huduma za jamii, Charles Nsanze amesema kila siku mwigizaji huyo atatumia saa nne kusafisha mazingira kisha ataendelea na shughuli zake nyingine za ujenzi wa taifa.

Atapumzika siku za Jumamosi na Jumapili au siku za sikukuu, hatakuwa peke yake kwa kuwa tayari hapa wapo wafungwa wengine tisa wanaofanya kazi za usafi wa mazingira”.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kuua bila kukusudia.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.