Mabeste Afunguka Mazito Kuhusu Mke Wake

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Mabeste amefunguka mazito na kumwagia sifa lukuki mkewe anayejulikana kama Lisa Fickenscher ikiwa ni siku ya kumbu kumbu yake ya kuzaliwa.

Mabeste na mkewe wamekuwa pamoja kwa kipindi kirefu sana na ni moja kati ya zile couple ambazo wamepitia mambo Mengi magumu maishani. Tangu Mabeste alipogombana na uongozi wake wa zamani mpaka alipougua ugonjwa wa ajabu lakini wameyavuka hayo yote na mpaka leo bado wako wote.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mabeste amefunguka na kusema kuwa moja kati ya vitu ambavyo hajutii kwenye maisha yake ni kumuoa;

Happy birthday my love sina kitu cha kusema zidi ya kusema nakupenda sana mama watoto wangu wewe ni mvumilivu sana una Upendo wa ajabu na una huruma pia, kikubwa zaidi una akili sanaa ooh thank you God kwa zawadi hii, kuna msemo unasema bora ukosee kujenga nyumba kuliko ukosee kuoa, yaani nakupenda sanaa sanaa kitu kingine kizuri ulicho barikiwa kikubwa sana, unapenda kazi yangu ya music unajua muziki mzuri ukisikia tu japo kuimba ndio hujui. Leo ni siku kubwa sana kwako na kwangu pia kwa sababu leo ndio naachia wimbo wangu”.

Lakini Mabeste hakuishia hapo aliendelea kumfungukia mkewe na kusema “Leo mama wa watoto wangu umezaliwa upya katika Bwana Yesu na pia hata kipaji changu kimezaliwa katika bwana wetu Yesu…kwenye Upendo sana Mungu yupo Muda wote”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.