Mabeste- Nimeamua Kufanya na Biashara Nyingine Maana Muziki Umekuwa Mgumu

Msanii wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Mabeste amefunguka Kuhusu uamuzi wake wa kutafuta kazi nyingine ya kufanya mbali na muziki ili kuweza kutanua wigo wake wa kupata kipato.

Siku za nyuma Mabeste alishawahi Kupitia wakati mgumu hasa lilipokuja suala la kukosa kipato kwani mke wake alipotwa na ugonjwa hali iliyopelekea wasanii kufanya Tamasha la kumchangia chochote kitu.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Risasi Vibes, Mabeste amesema amepitia mengi kwenye muziki lakini hawezi kuacha japokuwa ameamua kutafuta kazi nyingine ya kufanya ili kutanua wigo wa kujiingizia kipato.

Unajua kwa sasa wanamuziki wamekuwa wengi sana na changamoto zimeongezeka tofauti na ilivyokuwa mwanzo kipindi ambacho wanamuziki walikuwa wachache.

Sasa kwa wengine ambao tunaweza kuendelea na mambo mengine imebidi kujiweka kando kidogo huku tunafanya muziki lakini pia tunaendelea na maisha mengine, kwa sababu muziki ni kama zilivyo biashara nyingine.

Lakini limekuwa jambo la kawaida wasanii wa muziki kuanzisha biashara mbali mbali za pembeni za kuwaingizia kipato kwa kujua wazi kuwa hawawezi kufanya muziki milele hivyo inabidi upate kazi ya pembeni ya kufanya mbali na sanaa.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.