Madee Afunguka Usiri Wa Ndoa ya Dogo Janja.

Msanii mkubwa na maarufu bongo ambae amekuwa ni kama baba mlezi wa msanii Dogo Janja,Madeee amefunguka na kusema kuwa waliamua kufanya usiri aktika ndoa hiyo kwa sababu waliona kuwa endapo wangewashirikisha watu wengi inewezekana hata ndoa iyo isingefungwa kabisa kutokana na maneno ya watu.

Madee alisema kuwa alikuwa anajua kuwa wawili hao ni maarufu hivyo endapo wangetangaza ndoa hiyo ingeleta utata mkubwa na hata kuharibu kabisa mipango ya ndoa hiyo.

download latest music    

Nilijua ni habari kubwa, ni habari ambayo ingeleta purukushani kwa wanahabari hata ndoa yenyewe isingefanyika, na hata wale ambao tumewaalika tulijua hawa wana marafiki zao ambao ni wana habari, hivyo tulichokifanya ni kutengeneza usiri wa ile shughuli, hata tuliowaalika tuliwaambia mnakuja hapa lakini simu zenu wekeni hapa, unangia unashuhudia tukio lakini hauna ushahidi wa kupeleka kwa wengine”, amesema Madee

Madee anasema kuwa waliona hata haina haja ya kuwaalika watu wengi kwa sababu  inawezekana kila mtu angekuja na neno lake la kuwashauri na kutia doa ndoa hiyo.

Tungesema tuanze kuwaalika watu wangeanza kuwashauri ,ooh usikubali kuolewa na huyo au   kuoa huyo  ile ndoa ingekufa na tungepata dhambi.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.