Mahusiano Ya Joel Lwaga na Muna Hatiani Kuwaponza

Wasanii wa nyimbo za Injili Joel Lwaga na Muna wmedaiwa wapo katika hati hati za kufungiwa kufanya Muziki huo kutokana na kudaiwa kuweka kinyumba.

Global Publishers wanaripoti kuwa tangu msiba wa mtoto wa Muna utokee wiki chache zilizopita Kumekuwa na tetesi kuwa Muna na Joel wana uhusiano wa Kimapenzi.

download latest music    

Gazeti la  Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Rais wa Tanzania Music Foundation, Dk. Donald Kisanga wanaoshughulika na usimamizi wa waimbaji wa muziki wa injili ili kuujua ukweli na utaratibu ukoje kwa watumishi wa Mungu kama hao wanapotajwa kuishi pamoja kabla ya ndoa ambaye alisema kwamba wao wamekuwa wakisikia tu tetesi hizo lakini ukweli wake hawajaupata.

Tumekuwa tukisikia tu kwamba Joel na Muna wanaishi kinyumba lakini bado hatujapata ukweli wa hili jambo maana ni muda mrefu tunawaona wako kwenye kila huduma pamoja nasi tunawachukulia ni marafiki tu.

Dk. Kisanga alifungukia uwezekano wa wasanii hao kufungiwa kufanya Muziki wa Injili kama uhusiano huo upo kutokana na kwamba Muna ni mke wa mtu;

Sasa baada ya tetesi hizo kuzidi, kamati yetu ya maadili ipo kazini kwa sasa kufanya uchunguzi kama kweli wanaishi au walikuwa wanaishi pamoja au laa na endapo itathibitika kuwa ni kweli tutawafuta uanachama pia kuwafungia kuimba maana wanachafua waimbaji wote wa injili ambao wanaaminika ni watumishi wa Mungu.

Tunamshauri huyo Joel kuwa makini kama huyo Muna kweli ni mke wa mtu na hajapewa talaka aachane naye hata kama ni mchumba wake kama inavyosemekana kwani akiendelea kung’ang’ania itamletea matatizo“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.