Makabila Akiri Kuwa Anaenda Sana Kwa Waganga

Mwanamuziki wa muziki wa Kisingeli Dulla Makabila amefunguka na kukiri kuwa ni kweli ana tabia ya kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kunyoosha mambo yake.

Wasanii wengi wamekuwa wakisemekana sana kuwa wanaenda sana kwa waganga ingawa wengi wao wamekuwa wakikataa na kusema ni Habari za kizushi.

download latest music    

Lakini Makabila amekiri kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao wanaenda sana kwa waganga wa kienyeji na amechoka kudanganya kila siku akiulizwa.

Dulla Makabila amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online ambapo aliulizwa endapo Tetesi za yeye na wasanii wengine wa singeli kwenda sana kwa waganga ni za kweli:

Unajua mimi mtoto wa Kiislamu bwana nisiwe muongo kwa nini kila siku naulizwa hili swali siajua kwa nini wasanii wenzangu hawakutanagi nalo lakini mimi nakutana nalo kila siku siajua sijui sababu nahit ndio maana watu wanajua mimi naloga sana?.

Lakini kiukweli kabisa mimi kwa Mganga naenda na nikitoka hapa kwenyewe naweza nikapita na ninaamini katika hilo sijajua nyie wenzangu lakini mimi naamini Kwenye hili kama kuna watu nawakosea watanisamehe lakini mimi nimeshadondokea huko yaani ni bora nigombane na Mke Wangu lakini sio Mganga wangu”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.