Malaika Agoma Kumuanika Mpenzi Wake Licha Ya Usumbufu Mkubwa Anaopata

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na kibao cha ‘Rarua rarua’ Malaika amefunguka na kusema hawezi kumuanika mpenzi wake hadharani ingawa anapata Usumbufu Mkubwa kutoka kwa wanaume.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Malaika ambaye alijizolea umaarufu baada ya kusikika kwenye ngoma ya Chege ‘Uswszi Take away’ amefunguka kuwa hawezi kumuweka wazi mpenzi wake:

download latest music    

Siwezi kumuweka hadharani mpenzi wangu kwani Sidhani kama ni sawa kuweka kila kitu chako binafsi nje, maana wanachotaka mashabiki ni kazi yako na sio uhusiano wako.

Lakini pia Malaika amefunguka kuwa anapata usumbufu mkubwa kutoka kwa Wanaume hasa kwa sababu ya urembo wake:

Usumbufu upo mkubwa na ukizingatia ni msichana mzuri lakini hiyo haifanyi nimuweke wazi mpenzi wangu”.

Malaika ameongelea pia ukimya wake Kwenye tasnia ya Bongo fleva ambapo amesema alikaa kimya kwa muda kutokana na majukumu yake nje ya muziki.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.