Mama Ashura Ajikuta Katika Mgogoro Na Familia Ya Kiba.

baada ya tamasha la fiesta kufanyika jijini Dar Es Salaam, Mama Ashura ambae kwa muda mrefu amekuwa akitoa maoni yake ya kumkosoa msaini wa bongo fleva Alikiba ameibuka tena na kuongelea show aliofanya Alikiba usiku wa tamsha la fiesta lililofanyika pale Leaders Club.

Katika post yake ya kwanza msanii wa vichekesho nchini kutokea katika kundi la Timamu alisema kuwa  amekiona alichokifanya Alikiba katika fiesta na anatoa ushauri kwa Alikiba ili aache tabia ya kubweteka, huku akionekana kutoridhika na show ya msanii huyo aliofanya usiku ule.

download latest music    

Hata hivyo baada ya hapo Mama Ashura aliandika tena kwa undani kile alichokuwa anakimaanisha katika post yake ya awali aliyokuwa ameiweka katika ukurasa wake wa instagram.

Mama Ashura aliweka picha ya Alikiba tena na kusema kuwa watu wamekuwa wakimsifia Alikiba kutokana na kuwa na ufundi katika sauti yake lakini kumbe kuwez ku-win kimziki  hakutegemei ufundi wa sauti tu bali hata vile unavyoweza kucheza na muziki wako na kuangalia mahitaji ya muziki na mashabiki wako.Aama ashura hakuishia hapo lakini pia aliweza kutoa mfano wa msanii Diamond Platinumz kuwa ndie anaeweza ku-copy na sauti na crowd yake anapokuwa jukwaani.

Hii inakuwa sio mara ya kwanza kwa Mama Ashura kumuongelea Alikiba na hata kuwachana mashabiki wake, hatua ambayo ilifikia kuwa na vita ya kimtandao kati ya mama ashura na Team-Alikiba katika kurasa za instagram.

Baada ya kuongea hivyo, moja ya watu wa karibu wa msanii Alikiba , dada yake anaejulikana kama Zabibu Kiba alijibu maneno ya Mama Ashura kwa namna tofauti kidogo huku akificha kuonyesha nani katupiwa dongo hilo.Zabibu alioneshwa kukerwa na watu wanaokaa na kumpigia kelele  kaka yake ilhali yeye anaona kaka yake anafanya vizuri katika muziki.

ukijua nini unafanya na nani anakutafuta hata dunia nzima ikupinge, utazidi kusonga mbele tukatika mafanikio ili kufika unapotaka  sio kila mbwa anaekubwekea  unatakiwa kusimama na kupigana nae.

hata hivyo mpaka sasa ,Alikiba mwenyewe ajaongea kitu chochote kuhusu tuhuma izo ingawa ndugu zake wameingilia ugomvi huo.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.