Mama Kanumba Adai Anaogopa Maneno Ya Kejeli Kutoka Kwa Lulu

Mama mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Marehemu Steven Kanumba, Florah Mtegoa ‘Mama Kanumba’ amedai kuwa anahofia Elizabeth Michael ‘Lulu’ atamtolea maneno ya kejeli pindi atakapotoka jela.

Miezi michache iliyopita Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba.

download latest music    

Tangu Lulu amefungwa Mama Kanumba amekuwa akiongea mambo kadhaa kuhusu Lulu ambaye miaka michache nyuma alikuwa hana uhusiano naye mzuri sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Mwanaspoti, Mama Kanumba amefunguka na kudai kuwa hofu yake kubwa ni Lulu kumezeshwa maneno akitoka kuhusu na kuishia kumtolea maneno ya kejeli.

Mtoto wangu huyu anaweza kurudi mtaani na kushikwa masikio tena na watu kunifanyia vibweka kama alivyofanya awali, wala asithubutu wala kujihangaisha kwa kuwa iliyomshtaki ni Jamhuri hivyo anapaswa kuniheshimu. Hakuna neno lililoniuma kama siku aliyonipigia na kuniita kubwa jinga huku akiniambia haogopi polisi wala mahakama”.

Lakini pamoja na hayo Mama Kanumba amesisitiza kuwa hana bifu na Lulu wala kinyongo na atakuwa tayari kumtembelea jela kumsalimia kama ndugu zake watakuwa tayari.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.