Mama Kanumba Afunguka Kulizwa na Wema Sepetu

Mama mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Marehemu Steven Kanumba ‘Florah Mtegoa’, Mama Kanumba amefunguka na kudai kuwa Wema Sepetu amemfanyia kitu mbaya hakutegemea.

Mama Kanumba amedai kuwa hivi karibuni aliwasilisana na Wema Sepetu na kukubaliana wakutane na ndipo Wema alipomuita nyumbani kwake Salasala jijini Dar es salaam lakini amedai alipofika getini hakufunguliwa geti.

download latest music    

Inadaiwa kuwa majirani waliokuwa maeneo hayo walimuona mama huyo akiwa amesimama kwa muda mrefu bila kufunguliwa na wamekiri kuwa ni tabia ya Wema kutofungua geti la nyumbani kwake kama huna appointment yoyote kwake.

Kwenye Interview aliyofanya na gazeti la Ijumaa, Mama Kanumba alifunguka na kukiri kuwa jambo hilo lilitokea ambapo aliongea na Wema hivi karibuni kwa simu ambapo walikubaliana aende nyumbani kwake na ndipo alipokodi bajaji mpaka kwake na alipofika alikuwa akigonga geti walinzi walimwambia hawajapewa maagizo yake na alikuwa akimpigia simu hapokei.

Jamani inauma nyie mtu nimekubaliana naye vizuri unakodi bajaji mpaka kwake kulivyo mbali lakini hajali wala hapokei simu nikaamua kuondoka zangu”.

Mama Kanumba amedai kuwa walikuwa na maongezi ya kawaida tu kwani alikuwa mkwe wake na alikuwa anampenda lakini pia amefunguka na kusema amesikitishwa kwani mpaka hivi sasa hajaombwa radhi na Wema.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.