Mama Kanumba Akanusha Kuwa Na Kinyongo Na Lulu.

Kuna tetesi zimekuwa zikisambaa mtandaoni kuwa kuna chuki kubwa kati ya mma kanumba na msanii Lulu Michael kutokana na matukio ya nyuma yaliyotokea baada ya kifo cha Kanumba ambapo wengi walitegemea kuwa kungekuwa na uhusiano mzuri kati ya mama huyo na msanii Lulu Michael.

Wiki iliyopita mama huyo alifunguka katika vyombo vya habari na kuelezea na kulalamika kuwa Lulu Michael alikuwa akimtukana sana baada ya kutoka jela kwa mara ya kwanza ambapo alikaa kwa takribani mwaka mmoja kipindi upelelezi wa kesi yake ya mauaji ulipokuwa haujakamilika.

download latest music    

mama huyo kwa maelezo yake alionekana  kuwa na chuki na mwanadada huyo na hata kufikia hatua ya kusema kama atataka kwenda jela kumuona Lulu itabidi kwanza aongee na Mungu wake ili aweze kumruhusu kwenda kumuona msanii huyo.

Akiongea katika gazeti la Ijumaa Mama Kanumba anaejulikana kwa jina lake halisi Florah  Mtegoa amesem kuwa tabia ya watu kusambaza maneno na kusema kuwa ana chuki na lulu michael ni uongo kwa sababu yeye hana chuki yoyote na binti huyo na hivi karibuni akipata muda atakwenda kumuona msanii huyo gerezani.

Mama Kanumba anasema kuwa hata kama mahakama isingetaka kumfunga binti huyo bado kwake ingekuwa sawa tu kwa sababu hana lengo lolote la kumuumiza binti huyo na amekuwa akimchukulia kama binti yake.

Sina chuki na Lulu kabisa na tulikuwa karibu nae sana tu,lakini nafikia watu  watu wake wa karibu wanaomzunguka ndio wanaosababisha ukaribu wetu kuparanganyika sana.Lakini moyoni mimi nina mpenda sana Lulu , mimi nina imani ya kikristo kabisa, kwaiyo siwezi kufurahia kuona mwenzangu anapata matatizo , na ipo siku nitamtembelea gerezani.- Aliongea mama huyo.

Lulu alipata hukumu yake ya kuua bila kukusudia mwanzoni mwa mwezi Novemba , ambapo kifungo chake anatakiwa kukitumikia kwa miaka miwili baada kukutwa na hatia ya kumuua Kanumba.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.