“Mama Yangu Haniulizi Kama Natumia Madawa Ya Kulevya”- Chid Benz

Msanii wa Bongo fleva Rashid Makwiro maarufu kama chidi Benz amefunguka na kudai hawezi kuongelea suala lake la kitukia madawa ya kulevya kwa sababu hata mama yake mzazi hamuulizi mambo hayo na hawezi kumjibu.

Chidi Benz amekuwa muhanga mkubwa kutokana na kushindwa kujimudu kwa sasa katika muziki kutokana na athari alizozipata za madawa.
Chid kabla ya kujiingiza kwenye matumizi hayo, alifanikiwa kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa hapa nchini na kufanya vyema katika gemu la muziki.

download latest music    

Chid aliwahi kukiri kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya kupitia kituo kimoja cha redio hapa nchini katika siku za nyuma kwa kuomba msaada kwa ajili ya kujiondoa katika matumizi hayo jambo ambalo lilifanyika baada ya Babu Tale na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ kujitolea kumsaidia kwa kumpeleka katika Sober House ya Bagamoyo inayoitwa Life and Hope ambapo alikaa kidogo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Championi Chidi Benz aligoma kabisa kuongelea husu matumizi yake ya madawa ya kulevya na kudai kuwa hata mama yake mzazi hamuulizi :

Sitaki kuongelea kuhusu madawa ya kulevya kwa sasa, hata mama yangu mzazi haniulizi swali hilo kipindi hiki kwa sababu sitaki kusikia.

Hata aje mtangazaji kutoka BBC siwezi kumjibu swali hilo, kila siku unataka mimi niongelee kuhusu madawa ya kulevya, mambo ya madawa ya kulevya ni mabaya.

Naomba mniache mkae kimya kama mnavyokaa kimya kwa wasanii wengine ambao wanatumia madawa lakini hamuwaulizi.

Kama navuta ama sivuti niacheni mwenyewe. Nipo tayari kutoa ushirikiano katika kazi ya muziki, kwa sasa ninaendelea na kazi yangu ya muziki, nawaandalia mashabiki wangu nyimbo ambazo zitakwenda na wakati uliopo.”

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.