Mama’ake Rommy Atafuta Talaka BAKWATA

Mama mzazi wa Dj maarufu wa msanii Diamond Platinumz, Rommy Jones ambae pia ni kaka wa msanii huyo kutokana na ukaribu wao wa damu kwa sababu mama ya diamond na mama wa rommy ni mtu na dada yake, imesemekana kuwa amekuwa akienda   baraza la kiislamu (Bakwata ) kwa ajili ya kudai talaka kwa mume wake a nae ndoa miaka kadhaa iliyopita huku ikisemekana  kuwa mwanamke huyo anaejulikana kwa jina la Shani  amemzidi umri mwanaume wake,

Wakati huku ndoa ya mdogo wake ambae ni mama yake na Diamond(Sandra) ikiwa katika hatua za kuchipua huku kwa dada yake mambo ya ndoa yanaonekana kumshinda.

download latest music    

Dada wa mama Diamond (Shani) alionekana akiingia  Lakwata  mtaa wa lumumba jijini Dar kwa ajili ya kudai talaka kwa mwanaume wake ambae inasemekana kuwa alifunga nae ndoa miaka kadhaa iliyopitao lakini inasemekana kuwa mwanaume huyo ni mdogo kuliko Shani hivyo aliamua kuoa mwanamke mwingine anaeendana ane umri.

amekuja hapa mamaake na rommy anasema amechoka sana ,  mwanaume aliyenae amebadilika sana kwa sababu ameoa mwanamke mwingine wanaeendana nae umri,yeye ukimwangalia ni mkubwa sana kwa huyo bwana.Bakwata wamempokea na kumpa barua ya kwenda kumuita huyo mwanaume ili waje kuzungumza na ikibidi watoe talaka._Kilisema chanzo cha habari kilichokuwa kinapatikana maeneo hayo.

Hata hivyo wanahabari walifanikiwa kunasa barua hiyo ya Bakwata ambayo ilidai kuwa na muhuri na pia ilimtaka mwanaume huyo kufika ofisini hapo tarehe 27 February lakini siku ya tukio mwanaume huyo aliejulikana kwa jina la Ajazi alimuita mama huyo ofisini kwake na kumtaka wakayazungumze ili yaishe.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.