Mambo Ya Fashion Yataka Kumdhalilisha Wema Sepetu

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amedaiwa kutaka kudhalilishwa na fashion baada ya kutaka kudondoka Kwenye steji baada ya kuvaa viatu viewfinder na vyenye kisigino chembamba.

Global Publishers wanaripoti kuwa sakata hilo lilitokea wikiendi iliyopita mashindano ya Miss Morogoro 2018 ambapo alialikwa kama mmoja wa majaji.

download latest music    

Awali saa 6 usiku wakati Wema akiingia katika Ukumbi wa Hoteli ya Morogoro lilipofanyika shindano hilo alionekana akiwa amevalia gauni refu la rangi ya gold huku chini akiwa ametinga viatu virefu vilivyompa wakati mgumu kutembea kwa mikogo. Hata hivyo staa huyo alifanikiwa kufika kwenye meza iliyoandaliwa kwa ajili ya majaji na kukaa lakini shughuli ilikuwa pale ambapo alitakiwa kupanda jukwaa kutoa neno.

Wakati akielekea kwenye ngazi za kupandia jukwaani, Wema alionekana kuyumba na kutaka kupiga mwereka lakini mmoja wa watu waliokuwa karibu yake waliwahi kumzuia na ndipo aliposhikiliwa na kupandishwa. Hata hivyo, hali iliendelea kuwa tete baada ya staa huyo kufika ngazi ya pili ya jukwaa ambapo aliyumba tena na ndipo mtangazaji wa Redio Planet FM ya Moro, Warda Makongwa akaongeza nguvu na kumfikisha jukwaani salama.

Wakati wa kushuka ili kumuepushia aibu staa huyo, wadada wawili walionekana kumshika mikono na kushuka naye taratibu huku mtangazaji wa Redio Clouds FM, Gardner G Habash naye akiongeza nguvu. Mbali na viatu kumuumbua Wema, umbo lake namba nane lililokuwa limejengeka vilivyo kutokana na gauni alilokuwa amevaa lilikuwa gumzo na wengi waliibua gumzo kutokana na msambwanda wa mrembo huyo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.