Maneno ya Luge Mutahaba kwa Basila Mwanukuzi Yanatia Moyo.

Mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi kutoka Clouds Media Luge Mutahaba amefunguka na kumpongeza mwanadada Basila Mwanukuzi kwa kitendo cha kuamua kujitoa kwa ajili ya  mashindano ya Miss Tanzania ambayo yalikuwa yamefungiwa kwa takribani mwaka kutokana na kuwa na figisu nyingi.

katika mashindano hayo ambayo yalisubiriwa kwa muda mrefu  na kilele chake kufanyika siku ya Septemba 8 baada ya kuisha yalikuja maneno mengi ikiwepo ukumbi uliofanyikia mashindao hayo lakini pia zawadi ya gari ya mshindi ikipondwa sana na kusemekana kuwa haiendani na mashindao hayo .

download latest music    

katika ukurasa wake Luge aliandika ‘Basila Hongera sana mdogo wangu, kikubwa ulichofanikisha kufanya ni kuanza kurudisha imani kwa waliopoteza imani na hiyo brand. Sio siri, itakuchukua mwaka mmoja, miwili hata mitatu kufika kwenye level ya kupata the same integrity na value iliyokuwa imepotea. Kurudisha imani za wadhamini, wahisani na mwisho sisi wananchi tutarudi labda kwa ukubwa kuliko ilivyokuwa. Umefanya makosa mengi sana kwenye hii hatua ila ni sehemu ya ukuaji because najua hakuna mtoto anajaribu kutembea bila kuangukaanguka. Kama Clouds Media Group tupo na wewe na mawakala wote kwa pamoja mmewezesha jambo hili kurudi kupata heshima yake. Kubwa kuliko yote ili kujenga heshima inayodumu ungalizi wa washindi uendelee kwa muda mrefu kupata role models wengi kwa taifa letu. Mungu awabariki sana.”

Hata hivyo wapo waliokuwa wakimpongeza wengine kama Nikki wa Pili lakini pia wapo wengi waliomsema vibaya mwanadada huyo ambae pia aliwahi kuwa Miss Tanzania miaka ya nyuma na amejitahidi kwa mwaka huu kuyarudisha mashindano hayo kwa hadhi tofauti.

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.