Maneno Ya Rick Ross Kwenye Birthday Ya Diamond

Msanii mkubwa Duniani Rick Ross amepost picha  katika ukurasa wake wa Facebook kumpongeza msanii wa muziki wa Tanzania anaefanya vizuri Duniani kote Diamond Platinumz ambapo jana ilikuwa ni sikukuu yake ya kumbukumbu ya kuzaliwa.Diamond ambae kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha “Hallelujah” alichowashirikisha MorganHeritage

Hivi karibuni msanii Diamond alionekana katika baadhi ya post za Rick Ross akiwa kama mwakilishi mpya wa pombe ya Belaire kutoka Tanzania, kampuni ambayo Rick Ross pia anafanya kazi.Hivyo akiwa kama mwanafamilia wa Balaire Rick Ross aliamua kumpongeza msanii Diamond  kwa kazi nzuri anayoifanya  ya kutangaza kinywaji icho vizuri nchini Tanzania.Lakini pia amemkaribisha kwa mara nyingine tena katika familia ya wana Belaire.

download latest music    

Katika ukurasa wake wa Facebok Rick Ross aliandika ‘Happy Birthday to my brother Diamond Platinumz ,love how you have been reppin#belaire so with that said, Welcom  to the Belaire Family….#BlackBottleBoy”  aliandiak Rick Ross akiwa ameweka picha ya msanii Diamond katika ukurasa huo.

Ni kwa muda sasa kidogo tangu Diamond awe Ambassor wa kampuni ya kutengeneza vinywaji hivyo na amekuwa akijitaidi kwa kiasi kikubwa katika kufanya matangazo ya kinywaji hicho katika account zake mitandaoni.

Diamond ambae jana alishereka siku yake ya kuzaliwa, alianza kwa kutoa sadaka na misaada yenye thamani ya zaidi ya milioni  4 na kutoa zawadi mbalimbali kwa baadhi ya wagonjwa  katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar Es Salam . Diamond  akiwa kama mmoja wa watu waliozaliwa katika hopitali hiyo miaka kadhaa iliyopita aliamua kufanya hivyo kwa sababau anaamini kwamba wapo watu wengi maeneo  kama hayo wanaoitaji misaada, lakini pia msanii huyo anaamini kuwa hata waliopo hospitali pia ni mashabiki wa nyimbo zake , na hali hii ilijidhiirisha baada ya Diamond kufika hospitalini hapo baadhi ya kushughuli zilisimama kutokana na mashabiki kuwa wengi wakitaka kumwangalia msanii wao.

Bada ya shughuli hizo za mchana Diamond  alijumuika pamoja   na ndugu, rafiki  na jamaa zake wa karibu  katika kusherekea    sikukuu yake ya kuzaliwa.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.