Manfongo Akanusha Kukamatwa na Polisi na Matumizi ya Bangi.

Msanii wa muziki wa singeli nchini manfongo amakanusha taarifa zilizokuwa zikisambaa katika mitandao kuwa alikamatwa na kuwekwa ndani kwa muda na kusema kuwa wale walikuwa sungusungu ambao waliwakuta sehemu na kuwaomba pesa na walikata kutoa ndipo walipowapeleka kituo cha polisi.

Manfongo anasema kuwa katika eneo walilokuwepo kuna watu huwa wanavuta bangi hivyo walipoona na wao wamekaa maeneo hayo wakahisi kuwa ni kundi moja lakini hata baada ya kuwanusa mikono waliwachukua na kuwaomba ela na walikataa kutoa ndipo waliamua kuwapeleka polisi.

download latest music    

Sikukamatwa na polisi , wale walikuwa ni sungusungu ambao walinikuta maeneo ya Tandale, nilikwenda kwa kaka yangu kusalimia na walipokuja walinikuta tuko ndani na waliamua kutunusa mikono kama tunavuta bangi lakini waliamua kutukama na kutaka kutypeleka kituoni, yulikuwa njiani wakataka pesa na tulipowaambia hatuna wakachukua hatua ya kutupekea polisi.

Lakini pia Manfongo amekanusha taarifa za kua yeye ni mvutaji wa bangi kuwa sio za kweli hata kidogo.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.