Mange Ameanika Ukweli Wote Kuhusu Bifu la Diamond, Ruge na Kusaga

Mwanaharakati wa siasa mtandaoni mwanadada Mange Kimambi ameibuka na bomu jipya was huku safari hii akifunguka kuhusiana na mambo ambayo yanaendelea kati ya supastaa wa bongo fleva Diamond Platnumz na Wakurugenzi wa Clouds Fm Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.

Wiki iliyopita Diamond na Clouds Fm waliingia katika vita kali ya maneno ambapo meneja wa Diamond, Salaam SK alimtolea maneno mazito Ruge kwa kudai ana njama za kutaka kumuangusha Diamond na kumshusha kimuziki.

download latest music    

Leo Mange amefunguka na kudai kuwa ukweli kuhusu bifu hili unaanzia kuwa msanii Diamond yuko chini ya Ruge akimaanisha kwamba meneja halisi wa Diamond ni Ruge na Babu Tale na Salaam SK ni watu waliowekwa ili kuzuga watu wasijue kuwa Diamond yuko chini ya Clouds Fm.

Lakini pia Mange amefunguka na kudai kuwa sasahivi Clouds kuna matatizo makubwa kwani Joseph Kusaga anataka kuiuza Clouds kwa kuwa anafungua redio yake nyingine:

Joseph Kusaga anataka kuwekeza pesa yake sehemu nyingine na hiyo sehemu ni kwa Diamond kwa sababu basilica Clouds kuna matatizo makubwa, na Ruge amekuwa dizaini anamsumbua Kusaga kuhusu umiliki ukweli ni kwamba hakuna Clouds Fm bila Ruge”.

Lakini pia Mange amefunguka kuhusu umiliki wa mali za Diamond ambazo amedai zinamilikiwa na Joseph Kusaga:

Jamani ni hivi hiyo Wasafi Radio na Wasafi Tv, Joseph Kusaga ndio mmiliki wa asilimia 80% na Diamond anamiliki 20%  All the investment ya Wasafi Radio na Wasafi Tv amefanya Joseph Kusaga na pia hiyo Wasafi online 95% inamilikiwa na Kusaga lakini pia Chibu perfume 100% inamilikiwa na Joseph Kusaga na Diamond Karanga 100% inamilikiwa na Johanna Kusaga mke wa Joseph Kusaga”.

Mange amesisitiza kuwa hili bifu linaloendelea hivi sasa kati ya Diamond na Ruge ni kwasababu wanajua kuwa boss mkuu Kusaga yupo upande wa Wasafi na hivyo wakiwchana na Ruge Babu Tale na Salaam watakuwa mameneja wa Diamond full time.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.