Mange Ampa Mbinu Hizi Hamisa Ili Azikombe Pesa za Diamond

Mwanasiasa maarufu mtandaoni Mange Kimambi, ameibuka tena na jipya huku safari hii amempa mbinu mpya Hamisa atakazotumia ili aweze kupata pesa ya kulea mtoto wake kutoka kwa Diamond.

Tangu Diamond na Hamisa waweke wazi kuwa wamezaa mtoto kumekuwa na visa baada ya visa hasa baada ya Hamisa kudai kuwa Diamond amegoma kutoa pesa ya matumizi kwaajili ya malezi ya mtoto, kitu kilichopelekea Hamisa kumpeleka Diamond mbele ya sheria.

download latest music    

Baada ya habari kutapakaa kuwa familia ya Diamond inamkataa mtoto wa Hamisa na Diamond hataki kutoa pesa ya malezi, Mange ameibuka tena na safari hii kadai kuwa zari, Diamond na familia yao wanataka kumchosha Hamisa ili akate tamaa na kuifuta kesi yake mahakamani dhidi ya Diamond.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange alimpa mbinu hizi Hamisa ili aweze kupata pesa kwaajili ya malezi ya mwanawe.

Nimepitia kidogo sheria ya matunzo ya mtoto wa Tanzania inafanana na ya marekani, wanaangalia kipato cha wazazi na matunzo yanatolewa kutokana na kipato cha mzazi, ila tatizo wanawake Tanzania wanashindwa kuthibitisha kipato cha mwanaume mahakamani, Hamisa kama uyashindwa kupeleka ushahidi wa kipato cha Diamond utaishia kupewa laki mbili kwa mwezi. Kwanza ujue Diamond hawezi kutaja kipato chake cha kweli mahakamani inabidi umlazimishe”.

Pia Mange aliendelea kufunguka mbinu ambazo Hamisa atatumia kupata kipato halisi cha Diamond:

Ushahidi wa Kwanza ni uombe mahakama ikupe order ya bank account zote anazoweka pesa Diamond kuanzia mwezi wa 1 mwaka 2015, kampuni zote zilizoratibu show zake zote wapeleke order ya mahakamani wapeleke contract, kampuni zote zilizompa matangazo kama Danube na Vodacom na Diamond Karanga wote wachape barua za mahakama wapeleke mikataba.

Then peleka order ya mahakama kwa kampuni ya WCB na ile website yao wanayotunia kuuza nyimbo za wanamuziki na pia ichape barua ile Chibu perfume anayo share na Kusaga wote wachape barua waonyeshe mikataba yao na Diamond anaingiza shilingi ngapi. Ukitoka hapo wachape barua TRA kutoa rekodi ya malipo yake ya TRA”.

Mange alimalizia kwa kumshauri Hamisa asikate tamaa kumlea mtoto wake kwani kama alimpigania mpaka Diamond akamkubali mtoto wake hadharani basi aendelee kumpigania mpaka pale atakapokubali kumlea mtoto wake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.