Masanja Mkandamizaji Ajitapa Kuwa na Pesa Zaidi Ya Bakhresa

Msanii wa comedy na Mchungaji Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji ameibuka na kudai kuwa ana pesa nyingi Kuliko mfanyabiashara tajiri Bongo, Bakhresa.

Kwenye mahojiano na Kituo cha Clouds FM, Masanja amesema hawezi yakataa yale mazuri yanayozungumza na watu juu yake kwa kuwa midomo ya watu inanguvu sana kwaiyo anaamini kuwa yeye ni tajiri.

download latest music    

Kwa sababu ni jambo jema , unajua mtu akikwambia kuwa wewe unaoongoza kwa utajiri usikatae, ukikataa utakuwa umejikosea kwa sababu kitabu cha Mungu cha Biblia kinatufundisha nguvu iliyopo kwenye kinywa chako, kwahiyo mtu akisema kuwa mimi ni tajiri nitasema kuwa mimi ni tajiri ile mbaya na kwanini nisiwe tajiri wakati biblia inasema fedha na dhahabu ni mali ya baba yangu ninayemtumikia kwahiyo mimi kutumia au kumiliki vitu vya baba nimebarikiwa, ukiambiwa wewe ni tajiri usikae, ukikataa ina maana umeukataa utajiri’’.

Najisikia vizuri sana mtu akiniita tajiri na ulimi wangu lazima ukiri vitu vizuri kwahiyo ni kweli kabisa kama ambavyo wanasema mimi ni tajiri ile mbaya yaani Bakhresa anasubiri”.

Lakini pia Masanja Aliyah’s utajiri wake ikiwemo magari na majumba:

Nikwambie utajiri hautauhesabu kwa sababu ya kumiliki mjengo, ukimiliki mjengo ni sehemu tu ambayo Mungu amekubarikikwamba uwe unaweza kuwa na sehemu ya kuishi katikati ya watu wanaopanga, akikupa gari amekuhurumia tu kuepukana na mzunguko mingi ambayo ungetembea kwa miguu sasa unaweza kutumia usafiri kukurahisishia shughuli, utajiri wangu ni kuwa Yesu ambaye ana kila kitu, ukiwa na Mungu una kila kitu kwahiyo mimi ni tajiri zaidi matajiri kwa sababu nina kila kitu’’.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.