Mashabiki Wahoji Kiduku Cha Joti Kanisani

Ikiwa bado ndoa mbichi   na vyombo vya habari vikiwa vimechachamaa kusambaza picha za matukio ya harusi ya mchekeshaji mkongwe na balozi wa makampuni mengi nchini Joti, baadhi ya mashabiki na vyombo vya habari vimehoji muonekana wa bwana harusi tena hasa alipokuwa maeneo ya kanisani katika ndoa hiyo.

Joti ambae anamuonekana wa nywele za kiduku cha aina yake amefunga ndoa jumamosi iliyopita na mkewe huyu na sherehe kufanyikia akatika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Es Salaam.

download latest music    

staili ya nywele ya msanii huyo ambayo ni kiduku imekuwa ikiaminika kuwa ni fashion ya kihuni na sehemu za heshima haipaswi kuwepo hasa kanisani.sasa je joti ameruhusiwaje kufunga ndoa na style hiyo ikiwa ni staili ya kihuni na haikubaliki kimaadili.

Wakiwa kanisani , mmoja wa wahumini alisikika akinongona na mwandishi wa gazeti moja pendwa nchini”sasa hiki ndo kitu gani jamani, yanai kweli padri anaruhusu ili jambo lifanyikie kanisani kweli?

‘Huu mtindo wa nywele si mtindo wa viajana wa kihuni, wanaonyesha huko mtaani,wanaruhusuje hili jambo kanisani, au kwa sababu  huyo ni kijana maarufu’ mwanamke mmoja alisikika akisema pia.

Inawezekana ikawa ni kitu kidogo kwa baadhi ya mashabiki lakini, jotiambae ni balozi wa makampuni mengi nchi, muonekano wake ni biashara yake,hivyo yeye kubadilisha stle ya kunyoa kwa tukio la siki moja ilhali bado ana maeneo mengi ya kutumia muonekano huo ni vigumu .

Harusi ya msanii huyo ilifana sana baada ya joti kufunga ndoa na mkewe alikuwa mpenzi wake wa siku nyingi, waliohudhuria katika harusi hiyo walikuwa wengi akiwepo Mpoki na wasanii wote waliokuwa wakiunda kundi la ze comedy,Wolper, Steve Nyerere, Mboni Masimba na wengine wengi.

Muonekano wa Joti na mkewe wakiwa kanisani na ukumbini, Joti akiwa na kiduku. 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.