Mashabiki wamponda Diamond Platnumz baada ya kuonyesha cheni zake za mamilioni

Ni kweli kuwa Diamond Platnumz anapesa nyingi hadi imembidi kununua cheni na pete ambazo alilipia Tsh 158 millioni. Alipost picha hizi kupitia mtandao wake wa Instagram hata hivyo si mashabiki wengi walifurahia kitendo hiki na kuacha comments ambazo zilimfanya Diamond Kuwajibu.

Mashabiki hawa walionelea kuwa Diaomond Platnumz angetumia pesa hizo kuwasaidia maskini ambao hawana hata nyumba za kuishi wala chakula cha kula. Diamond na yeye pia aliwajibu kwa kuwatajia mambo ambayo ameweza kufanya kuisaidia jamii ili kuwajulisha kuwa hakuwa mtu selfish.

Aliandika kusema…

download latest music    

Nimejenga nyumba 5 mwaka janaIringa, Misikiti miwili mmoja Morogoro pia nyingine Mtwara na Madrasa tegeta na nyumba ya Imamu mbili na sadaka mbali mbali sasa unataka nitoe ela zote sadaka nami nisifurahishe nasfi? Hebu niombe radhi kwa hilo.

Comment yake ata hivyo haikuwafurahisha mashabiki hao waliondelea kumponda na kumwambia kuwa amekuwa mtu mwenye kiburi na kuwa amesahau alikotoka. Je wewe waonaje?

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua