Mashabiki Wamshambulia Irene Kisa Ugonjwa wa Dogo Janja

Mwanadada Irene uwoya amejikuta katika wakati mgumu baada ya mashabiki zake na mashabiki wa mume wake Dogo janja kumshambulia kwa maneno katika ukurasa wake wa instagram kutokana na kuumwa kwa Dogo janja.

Dogo Janja ambae alionekana akiwa hospitali wikiend hii  lakini inavyosemekana ni kwamba mwanadada huyo hakuwa anaonekana maeneo ya hospitali huku akipost picha yuko sehemu nyingine kabisa ikionekana ni sehemu ya starehe.

download latest music    

Hata hivyo wawili hao wameonekana kuwa hawako karibu sana kama zamani, lakini kila mmoja anapooulizwa kuhusu mahusiano yao wamekuwa wakisema kuwa kila mtu ana ratiba na kazi zake hivyo hawawezi kuharibiana ratiba.

Dogo Janja ambae anasemekana kusumbuliwa na matatizo ya kupumua  kwa shida na pia kupungukiwa na maji anasema kuwa hakuna watu wanaojua zaidi ya ndugu zake huku akisherekea sikukuu yake ya kuzaliwa akiwa hospitalini hapo.

mpaka sasa hakuna mtu anaejua zaidi ya watu wangu wa karibu tu, lakini pia naomba mashabiki zangu waniombee tu niwahi kupata nafuu na kutoka humu maana wala sitamani kukaa humu.

Hata baada ya kuweka post yake akiwa anaumwa watu mbalimbali wameenda katika ukurasa wa Irene uwoya na kumsema kuwa hamjali kabisa mume wake ambae yuko hospitali ana kazi ya kufanya mambo mengine tu Binafsi.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.