Mashabiki Waombwa Kumsaidia Hawa wa Nitarejea

Kama mwaka sasa umepita tangu mwanadada hawa alipowahi kutolewa katika vyombo vya habari kuwa alikuwa amekuwa kama teja kutokana na matumizi ya pombe za kienyeji zilizompelekea pia kuacha muziki na kujikuta akibaki nyumbani tu,

Baada ya hapo walimsaidia dada huyo na kwenda sober ambapo alipatiwa matibabu na kuanza kurudi katika hali yake ya kawaida lakini bado alikuwa akihitaji msaada wa hapa na pale ili kurudi kimuziki.

download latest music    

Sasa mapya ayameibuka kuhusu hali ya mwanadada huyu huku akionekana kuendelea kudhoofka kabisa  na hii yote ni kutokana na ukweli kuwa mwanadada huyo kwa sasa ni mgonjwa sana na amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa ini unaoendelea kutafuna sana afya yake.

Soudy Brown wa kipindi cha shilawadu kutoa Clouds Media amethibitisha ilo baada ya kwenda  kumtembea mwanadada huyo huku akionekana kudhoofika sana na hali yake aliyonayo kwa sasa.

Mwanadada huyo anaomba msaada kwa watu mbalimbali kwa chochcote kwa sababu ya matibabu na pia hata familia yao pia haina uwezo kwa kutoa huduma ya kila kitu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.