Mashabiki Wapata Wasiwasi Utetezi Wa Lulu Mahakamani

Ikiwa bado kesi inaendelea na utetezi ukizidi kufunguka mahakamani,  jana msanii Elizabeth Lulu Michael alipata nafasi ya kutoa ushahidi na kujitetea kabla ya kupewa hukumu ya kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili.Hata hivyo baadhi ya mashabiki wake katika mtandao wa instagram wamekuwa wakitoa comment zenye kuonyesha  mashaka yao juu ya utetezi wake na kwamba inawezekana wakampoteza msanii wao.Katika baadhi ya utetezi wake ambapo baadhi ya mashabiki wake wanasema kuwa lulu ameanza kutia mashaka katika kutoa ushahidi huo kwa sababu baadhi ya maneno aliyoyatoa yanakuwa yakitia wasiwasi ingawa maamuzi na hukumu ya kesi iyo iko mikononi mwa mamlaka ya mahakama.

mashabiki wamekuwa wakioji, kama kweli lulu alikuwa akipigwa na marehemu mbona hakuwahi kutoa ushahidi wa kipigo chochote alichowahi kupigwa, na je kama siku ya tukio alipigwa na panga kama alivyosema mbona hakuna uthibisho wa alama za kipigo hicho, je kwanini baada ya mpenzi wake kudondoka  Lulu aliondoka na kuelekea coco beach ambapo baadae ndipo alipokamatwa na polisi.Hayo ni baadhi ya maswali na mashaka ambayo mashabiki wake wamekuwa wakijiuliza na kufikia hatu aya kuacha majaji kuamua kesi iyo.

download latest music    

Akiwa kama kijana na msanii ambae ndio anaelekea kufanikiwa zaidi katika kazi zake , Lulu anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia ,tukio lililotokea miaka minne iliyopita baada ya kutokea kifo cha mpenzi wake Steven Kanumba.Steven Kanumba alikuwa moja ya wasanii wakongwe waliojitolea kufanya tasnia ya bongo movies kukua.

Hata hivyo, kama mashabiki na familia na watu wa karibu wa msanii huyo, bado hawapaswi kuonyesha wasiwasi ,zaidi ya kumtia moyo na kumuombea kesi ipite, kwa sababu mwisho wa siku  waliokuwepo katika tukio ndio wanaoweza kusema kilichotokea na Lulu ni mmoja wa watu hao na uamuzi wa mwisho siku zote utolewa na mahakama.

kwa muda huu Lulu hapaswi sana kujikita ktika mitandao ya kijamii kwa sababu kuna mngi yanayozunguka ambayo yanaweza kumuongezea matatizo zaidi. TUNAMTAKIA KILA LNEYE KHERI KATIKA HILI!!!

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.