Mastaa Waendelee Kujisitiri Kama Mwezi Mtukufu-Shamsa Ford

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amewataka wasanii wenzake kuendelea na kufanya mema waliyokuwa wanafanya kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda Shamsa alisema ndani ya mwezi wa Ramadhani watu mbalimbali hasa mastaa walikuwa wakiuhesh­imu kwa kufanya yaliyo mema, kuvaa kiheshima na kutoachia video na picha za ajabu mitandaoni hivyo hata sasa waendelee hivyo hivyo ili kuendelea kumtukuza Mungu zaidi.

download latest music    

Nawasihi mastaa waendeleze mema waliyokuwa waki­yafanya wakati wa Ramadhani, tusione wakiwa wanakaa nusu utupu au kufan­ya mambo mengine ya ajabu, wafanye ibada sana maana maisha yenyewe ni mafupi mno”.

Mwezi Huu wote ulikuwa ni mwezi mtukufu ambapo waislamu walikuwa wanafunga na kuomba kwa Imani zao na kufanya mema na hata mavazi yao yalikuwa yakujisitiri sana tofauti na siku za nyuma.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.