Matonya Afungukia Tetesi za Kuuza Madawa Ya Kulevya

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Matonya amefunguka na kukataa kata kata skendo za yeye kujihusisha na kuuuza na kusambaza madawa ya kulevya huku akiziita ni fununu tu.

Kipindi cha nyuma kuna stori za Matonya kuuza madawa ya kulevya zilisambaa sana hadi kuna muda kuna taarifa zilidai kuwa aliwahi kukamatwa nchini China akiwa anasafirisha.

download latest music    

Sababu kubwa iliyopelekea taarifa hizo kuenea hivyo ni sababu ya maisha aliyokuwa anaishi kwani alikuwa hafanyi mziki kwani alikuwa hana nyimbo yoyote iliyokuwa inahit kwenye redio wala Tv na hata shoo alikua hafanyi lakini bado alikuwa anaishi maisha mazuri.

Alikuwa mtu wa kuishi maisha ya hali ya juu alikuwa anaendesha magari makali alikuwa ana nyumba ya kifahari lakini pia kuna taarifa zilienea kuwa alikuwa anaishi na mwanamke huko Moombasa ambaye alikuwa anamuweka mjini lakini baadae akapata bonge la skendo la kutumia madawa ya kulevya.

Matonya amefunguka taarifa hizo Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv na kukataa habari na kusema mambo ya madawa ya kulevya zilikuwa ni fununu tu:

Kiukweli hata mimi nasikitika kwani sio mimi tu hadi familia yangu hasa mama yangu kipindi hicho cha iyo vurugu alikuwa ana wasiwasi alikuwa ananipigia simu kila saa na haamini kama ni mimi kwani watu waliharibu kila mahali watu walizusha kuwa nimeshikwa China nataka kunyongwa lakini kikubwa ninachotaka kukisema kuwa hizo ni stori tu za mtaani ni fununu”.

Lakini pia Matonya amefunguka kuhusu taarifa za yeye kuwa na bifu na Ali Kiba ambazo amedai ni stori tu ambazo watu wamekaa wametunga kwani yeye hana bifu na mtu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.