Maua Sama Afuata Nyayo Za Rostam Kwa Hili

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini aliyofanya vyema na ngoma yake ya ‘Iokote’ Maua Sama amefunguka na kuweka wazi anaunga mkono msemo wa wakali wa Hip Hop Roma na Stamina (Rostam).

Roma na Stamina Wameunda msemo wao wa ‘Tunafunga Jumla jumla’ kwa ajili ya kuufungia mwaka 2018 kikazi zaidi kwa njia ya Sanaa ya muziki.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Maua Sama anayetamba na Ngoma ya Iokote alisema kuwa, ametokea kuvutiwa na msemo huo baada ya kuusikia na kwamba anatamani kuja na wimbo wenye jina hilo.

Nimependa kwa kweli, kwa sababu msemo kama huu kutumika mwishoni mwa mwaka huwa mzuri, unaweza kuta mtu umefanya biashara zako sasa unafunga jumla jumla ili ufungue mwaka mwingine.

Nitajaribu kuongea na Rostam ikiwezekana nitatoka na wimbo wa tunafunga jumla jumla baada ya hii ya Iokote”.

Maua Sama licha tu ya kuvutiwa na msemo wa Roma na Stamina ‘Tunafunga jumla jumla’ na kutaka kufanya wimbo Lakini pia wasanii hao wametangaza kufanya baadhi ya shoo pamoja.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.