Maua Sama Atembea Kifua Mbele kwa WCB.

Mwanadada Maua Sama ameonyesha juhudi zake mbele ya wasanii wengine baada ya wimbo wake wa iokote kufanya vizuri  katika mitandao na station mbalimbali za burudani.Maua ambae hivi karibuni amekuwa katika wakati mgumu kutokana na kuweka rumande kwa zaidi ya siku tano anaonyesha kufurahishwa na jambo hilo.

Wimbo wa Iokote ndio uliomfanya Maua  kuwekwa rumande kutokana na hisia za mashabiki katika wimbo huo na kushtakiwa kwa kosa la kudharirisha pesa ya Tanzania.

download latest music    

Hata hivyo tangu akiwa bado polisi rekodi ya wimbo huo kufanya vizuri ilikuwa ikionekana na  mpaka sasa wimbo huo unaonekana kuendelea kufanya vizuri  na kuwashinda wasanii wa WCB na nyimbo zao mpya ambazo nyingi zimetoka hivi karibuni.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.