Maua Sama Kufunga Ndoa Mwakani

Ndoa ni jambo la kheri sio kwa mwanamke tu, ila hata kwa wanaume, wasanii wengi wa Bongo wamekuwa hawadumu katika mahusiano na kuachana kila baada ya miezi michache,hii imefanya wasanii wengi washindwe kuingia katika ndoa , bado sababu haiko wazi lakini ni wasanii wachache wenye kukaa kwenye mahusiano kwa muda mrefu  na kufikia hatua ya  kufunga ndoa.

Mwanadada mrembo kabisa katika tasnia ya  muziki wa Bongo fleva nchini, Maua Sama ambae kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha” Katukatu’ amefunguka na kusema kuwa ndoa yake na mwanaume aliyemchumbia hivi karibuni inaweza kufanyika hapo mwakani lakini kwa sasa bado kidogo mipango  ya harusi haijafanyika.Msanii huyo ambae miezi kadhaa hivi iliyopita alichumbiwa na mchumba wake mwenye asili ya kizungu anasema kuwa wanatarajia kufunga ndoa mwakani.

download latest music    

Maua Sama akiongea katika Over the Weekend ya gazeti la Ijumaa, alisema kuwa ana uhakika michongo yote ya harusi itaenda vizuri lakini kwa utaratibu wake na kazi zake kwa sasa  hana mpango wa kufunga ndoa  mwaka huu hadi mwakani.’Bado sana mipango ya ndoa kwa sasa mpaka mwakani.Sasa hivi ninaangalia zaidi muziki wangu,” aliongea Maua

Hata hivyo msanii Maua anasema kuwa anamshukuru sana Mungu maana ameweza kumsimamia na kuweka kukaa kwenye game muda mrefu huku nyimbo zake zikifanya vizuri ,lakini pia ameelezea sababu za msanii kukaa katika game la muziki  kwa muda mrefu ni vile ambavyo msanii anaamua kujiweka  “nashukuru nimeweza  kukaa kwa muda mrefu  bila kuchuja  na hii ni kutokana  na hii ni kutokana na msanii unavyojiweka” aliongezea Maua

Maua SaMa ambae pia ni zao zuri kutoka katika jumba la kulea wasanii wenye vipaji  nchini la THT , amekuwa mmoja wa wanadada wanaofanya vizuri kuanzia katika wimbo wake wa ‘Mahaba niue’ ambao ulikaa muda mrefu kwenye chati, lakini hata baada ya wimbo huo nyimbo zilizofuata ziliendela kufanya vizuri na kupokelewa vizuri na mashabiki wake, akiwa pia ni mmoja wa wasanii wanaozunguka mikoani katika tamsha la Fiesta , maua amekuwa akipokelewa vizuri katika jukwaa la Fiesta.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.