Mboso Ashusha Lawama kwa Mashabiki

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Maromboso au maarufu kama Mbosso ameelekeza lawama kwa mashabiki baada ya video yake kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Siku chache zilizopita video ilisambaa mtandaoni iliyomuonyesha Mbosso akiiwa stejini akitumbuiza kwenye shoo ya Kusi night huku akimbambia msichana mmoja katika staili za kimahaba.

download latest music    

Video hiyo ilisababisha mashabiki kumjia juu Mbosso huku wakiwarushia lawama WCB na kudai wamembadilisha Msanii huyo na kumfundisha tabia mbaya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Mbosso amefunguka hay kuhusu video ile:

Unajua watu wengi wanaamini mimi nimebadilika lakini hakuna kuna baadhi ya vitu vinachangia hasa kwenye shoo inakulazimu ufanye vitu fulani ili watu wafurahi kwaiyo unajikuta unafanya vitu fulani ili shoo ipendeze na watu wafurahi na mashabiki wawe na shangwe na wewe ndio inabidi uwape burudani mashabiki  zako”.

Lakini pia Mbosso amesisitiza kuwa yeye binafsi hakupenda kufanya vile ila kutokana na msukumo wa mashabiki waliokuwa wanampa ukumbini pale akajikuta akifanya vile.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.