Mbosso-Kuna Media Zilitaka Kunizika Nikiwa Hai

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka WCB anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Nadekezwa’ Mbwana Yusuf maarufu kama Mbosso amefunguka na kudai kuna kipindi baadhi ya media zilikataa kucheza kabisa nyimbo zake.

Mbosso amedai jambo hilo lilimkuta alipotoka katika kundi la Yamoto na kuwa Msanii wa kujitegemea ndipo alipokutana na vikwazi vya baadhi ya media kugoma kabisa kucheza nyimbo zake.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mbosso alisema kwamba kipindi hicho kilikuwa ni kigumu kwenye maisha yake, kuna muda alikuwa hadi analia, lakini baada ya kuingia WCB, mambo yamebadilika kabisa na kila siku anaona muujiza mpya kwenye kazi yake ya muziki.

Kiukweli ninamshukuru Mungu anayetoa riziki. Ingekuwa inatolewa na binadamu pengine mimi nisingepata chochote kwa sababu kuna baadhi ya media zilikuwa hazichezi ngoma zangu, zilitaka kunizika nikiwa hai zikiamini kwamba siwezi na sitafika popote pale.

Lakini Mungu mkubwa, mambo yamebadilika na kwa sasa nipo kazini ninafanya kazi na wanamuziki watano wakubwa Afrika, na kila kitu kikikaa sawa nitaweka wazi”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.