Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia aambia Bunge Diamond amekwepa kulipa kodi

Ni miezi mbili tu iliyopita ambapo Diamond alienda kwa makao makuu ya Mamlaka ya Mapato TRA baada ya kuitwa ili alelezee namna anavyopata mapato yake na namna gani analipa kodi ya serikali.

Diamond alipewa cheti na TRA kama dhibitisho kuwa analipa kodi ya serikali kama inavyohitajika na sheria ya Tanzania.

download latest music    
Diamond alipoitwa kwa makao makuu ya Mamlaka ya Mapato TRA

Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia hata hivyo jana aliambia Bunge kuwa Diamond anadaiwa na Mamlaka ya Mapato zaidi ya shilingi milioni 400.

Mheshimiwa Mtulia alidai kuwa hit maker huyo wa ‘Marry You’ alimwambia kwa sasa anadaiwa kodi ya zaidi ya shilingi milioni 400 na TRA.

Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia

Mbunge huyo aliyasema hayo wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ulipokuwa ukijadiliwa bungeni.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere