Mc Pili Pili Aruhusiwa Kutoka Hospitali

Mshehereshaji maarufu Emmanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili ameruhusiwa kutoka hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza baada ya kulazwa kwa takribani siku nane.

Daktari bingwa wa upasuaji hospitalini hapo, Hans Klaud ambaye pia amekuwa akimpa huduma za kitabibu anasema wameridhishwa na hali ya mgonjwa wao kabla ya kumruhusu.

download latest music    

Mkali huyo wa kuvunja mbavu alilazwa hospitalini hapo Bugando mara baada ya kupata ajali ya gari lake binafsi Septemba 12 mwaka huu mkoani Shinyanga.

Hata hivyo Mc Pilipili amepata amepata majeraha ya kifua, kichwa na kiunoni hali iliyowalazimu wataalamu wa afya hospitalini Bugando kumfanyia vipimo vikubwa ikiwemo CT scan na Chest scan ili kubaini kama amepata madhara kwa ndani. Vipimo hivyo vilirejesha majibu chanya kwamba Mc Pilipili hakuumia kwa ndani bali alipata majeraha tu, yaani external injuries.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.