Mc Pilipili Atamani Kuoa Baada Ya Kuona Joti Kaoa

Msanii wa maigizo ya uchekeshaji  Mc Pilipili amefunguka na kusema kuwa hata yeye ametamani sana kuoa baada ya kumuona msanii mwenzie wa maigizo ya vichekesho  Joti kuwa ameoa lakini kuna baadhi ya mambo yanayomtilia vikwazo katika ndoa yake .

Msanii Joti ambae amekuwa ni mmoja wa wasanii wa maigizo ya vichekesho alifanikiwa sana katika kazi yake na kwa sasa amekuwa ni moja ya mabaolozi wakubwa wa makampuni mbalimbali nchini ameoa weekend iliyopita ya tarehe 28 Oktoba na harusi kufanyikia Mlimani City jijini Dar Es Salam.

download latest music    

Nilipenda sana kuoa mwaka huu  tena hasa mwezi huu wa kumi  ila imeshindikana kwa sababu mpaka mwezi wa kumi umefika bado sijapata mchumba wa kumuoa, lakini  mpaka mwezi wa kumi mwakani ninaamii kitu kikubwa sana kitatokea” alisema Mc Pilipili.

Hata hivyo Mc Pilipili anawapa tahadhari wadada wa mjini mabao wamekuwa wakiona dharau sana kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa wasanii wa maigizo ya vichekesho na kusema kuwa hata wao pia ni watu, kauli hii inajirudia tena kwa baadhi ya wasanii wa vichekesho .

Moja wa wasanii wa vichekesho anaejulikana kama Mkali Wenu alishawahi kutoa lawama hiyo na kusema kuwa wdada wengi wamekuwa hawachukulii umakini pale wanapofatwa na wasanii wa maigizo ya vichekesho kwa ajili ya mahusiano, inakuwa kama wanawatania kumbe wao wanakuwa serious na maneno yao.

Mc Pilipili ambaye anasema mpaka sasa hajapata mchumba alishawahi kuwa katika mahusiana ya kimapenzi na wasichana maarufu Tanzania kama Nandy ambae ni msanii na anafanya vizuri katika game na pia alishawahi kutoka na Nicole Franklin amabye alishawahi kutwaa taji la Miss Shinyanag 2014.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.