Mchumba Wa Wolper Amedai Alikuwa na Uhusiano na Wolper Wakati Yupo na Brown

Sadick Athanas Sanga ‘Engine’ ambaye ni mchumba wa muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Jacqueline Massawe ‘Wolper’ amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake na mrembo huyo.

Wolper aliuanza mwaka kwa kutawala kwenye midomo ya watu na kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutangaza kuchumbiwa na mpenzi wake huyo, lakini kilichowafanya watrend zaidi ni habari za kudai kuwa mwanaume huyo alifanya kufuru kijijini kwa kina Wolper kwa kujaza magari ya kifahari.

download latest music    

Tangu habari hizi zimeanza kuenea kuna mambo Mengi ambayo yamekuwa yakizunguzumzwa kiasi ya kwamba ameamua kufunguka yote kwenye mahojiano yake na Millard Ayo TV:

Mimi nimeshamchumbia Wolper na nimeshatoa na mahari yaani kila kitu nimeshakamilisha na tulizungumza tukakubaliana kwa muda mrefu na hatimaye tukafika hatua hii. Nimekuwa na mahusiano na Wolper kwa siku kwaiyo alivyokuwa na mtu mwingine nilimpisha aendeleenam mambo yake lakini walivyoachana na mimi nikachukua nafasi na tunaelekea kufunga ndoa sasa”.

Mume huyo mtarajiwa wa Wolper amesisitiza kuwa hana mpango wa kuanika taarifa zote kuhusu mahusiano yao kwenye mitandao ya kijamii ila tu  amesisitiza kuwa ndoa yao ambayo itafungwa hivi karibuni haitahusisha michango ya watu bali kutakuwa na mialiko tu.

Lakini pia mchumba wa Wolper amesisitiza kuwa taarifa zilizosambaa kwenye mitandao kuwa ndoa yao ya ghafla sio kweli kabisa kwani penzi lao halijakuwa kama uyoga bali walianza siku nyingi na mipango mingi imehusika.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.