Meneja Maneno Amtetea Duma Kuhusu Swal la Ushirikina.

Meneja wa msanii wa bongo movies David maarufu kama Duma amefunguka na kutoa utetezi wake kwa msanii anaemsimania na kusema kuwa pamoja na kwamba watu wamekuwa wakisema kuwa msanii wake amekuwa akitumia ndumba lakini yeye anachoamini kuwa anachopitia Duma sasa hivi ni wakati wa mungu na wala sio kitu kingine kama watu wanavyosema.

Akiongea na EATV , meneja Maneno anasema kuwa pamoja na yote yanayoendelea kusemwa lakini anaamini kuwa kujituma ndiko kunakoleta mafanikio.

download latest music    

Tuhuma za ushirikina zipo maana huwezi kuwakataza watanzani kusema yale wanayoyasema hata siku moja, na ikifika siku Duma akifanikiwa watasema kuwa Duma ni Freemasons na kuongelewa mengi juu yake, lakini tu unapokuwa maarufu kuongelewa kupo na ni kawaida.

Hata hivo meneja maneno anasema kuwa amegundua kuwa tasnia ya filamu inahitaji mabadiliko makubwa na mabadiliko hayo hayawezi kuja kama hakutatumika nguvu kubwa na nyingi kwa ajili ya kufanya hivyo na ndio maana yeye ameamua kujikita na kufanya kaz na Duma ili kufanikisha hayo.

Meneja huyo anasema kuwa pamoja na kwamba watu wamekuwa wakienda kwa waganga kuloga lakini mwisho wa siku unachotakiwa kujua ni kwamba hata waganga pia wanamtegemea mungu vilevile.

kwa mganga ni kama nyumba tu au gheto unakwenda unapiga stori tu fresh,nilikuwa sijajua kuwa kumbe hata mganga pia ana,tegemea mungu kwa sababu angekuwa anatumia nguvu zake basi angesababisha watoto wak waolewe na mawaziri na matajiri lakini mwisho wa siku wote tunabaki  kusugua rumba na kunyunyiza dawa.kwaio ukimuamini Mungu unafanikiwa kila kitu na ninachoamini kuwa Duma anachofanya kwa sasa ni wakati wa Mungu.”

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.