Meneja Wa Diamond Ahaidi ‘Kumuanika’ Ruge Endapo Atamuandama Tena Diamond

Sakata linaendelea kupamba mtoto kati ya meneja wa Diamond Platnumz Salaam SK na timu nzima ya WCB dhidi ya Ruge ambaye ni Mkurugenzi wa vipindi Clouds Media.

Kizazaa hiki kilianza wiki iliyopita kutoka kwa vijana watangazaji wa kipindi cha Shilawadu Qwisa na Soudy Brown ambao walidai kuwa wamepewa kichapo cha hali ya juu na mcheza shoo wa WCB Mose Iyobo.

download latest music    

Ambapo inasemekana kuwa walimfata Aunty Ezekiel ofisini kwa kwake kwenda kumfanyia mahojiano kuhusiana na suala la ugomvi wao na Tunda lakini kwa bahati mbaya hawakumkuta lakini badala yake walimkuta Mose Iyobo ambapo walidai baada ya kumuuliza maswali mawili matatu aliwageuzia kichapo na kuuanza kuwapiga na kutaka kuwagonga na gari hali iliyowasababishia majeraha.

Tangu siku hiyo kumekuwa na maneno mengi yanayoongelewa mtandaoni lakini hali ilikuwa inaonekana kama si shwari kati ya WCB na Clouds ambapo jana walitoleana povu zito ambapo Meneja wa Diamond anayejulikana kama Salaam Sk amedai kuwa kuna njama zinapangwa ili kumshusha Diamond kimuziki.

Diamond Platnumz na Uongozi Wake

Sallam Sk alifunguka na kudai kuwa Shilawadu hawakupigwa na Mose Iyobo kama walivyodai bali walimtumia Mose ili kumharibia Diamond kwenye jamii na timu nzima ya WCB hivyo akadai kuwa atamuanika Ruge na maovu yake yote ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:

Kwa heshima ya bwana Joe Kusaga kukuombea msamaha leo Bwana Ruge Mutahaba naamua kukusitiri ila ukiendelea kuyafanya ambayo unayafanya basi ntayaanika maovu yako yote unayofanya kwenye Industry ya muziki. WCB haina tatizo na media yoyote na wala haina tatizo na Clouds media group ila huyu Ruge ndio mwenye matatizo #tumekataakuwakaa”.

Mpaka sasa sio Ruge wala Clouds waliotoa tamko lao rasmi kuhusu sakata hilo lakini kuna habari za chini chini zinazodai kuwa hii yote ni kiki tu iliyopangwa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.