Mfahamu Video Queen wa Kwanza wa Diamond Katika Wimbo wa Nenda Kamwambie.
Ni mika mingi imepita tangu diamond atoe wimbo wa nenda kamwambie ambaop ndio wimbo wake wa kwanza na uliomtambulisha katika tasnia ya mzuki. lakini inawezekana kabisa ni wachache wanaomjua yule video queen aliyewahi kutokea katika wimbo wake ule wa kwanza.
Basi siri kubwa mabyo inawezekana ni wachache wanaijua na inawezekana wengi hawakuwahi kuigundua ni kwamba mwanadada ambae ni video queen kwenye video ile ni dada yake kabisa na Diamond anaejulikana kama Esma Platinumz kwa sasa.
Akitoa sababu ya kumtumia Esma, Diamond aliwahi kusema kuwa kipindi kile alikuwa hana pesa na wadada wengi walimlingia na kukataa kufanya nae video kwa sababu halikuwa hana pesa na walikataa kufanya bure hivyo ilimlazimu kufanya na esma kuepusha gharama.
Lakini ndio huyo Diamond ambae sasa kila mtu anatamani kufanya nae kazi, hata siku moja upaswai kumdharau mtu usiyemjua na kujua kusudi la mungu ndani yake.