Mh. Mwakyembe Kupitia Upya Mikataba ya Mzee Majuto.

Baada ya kutangazwa katika vyobo vya habari kuwa msanii mkongwe nchini mzee majuto ni mgonjwa sana na aanahitajika kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu kuhu akiomba msaada wa kupewa fedha za matatibabu, mh waziri anaeshughulika na maswala hayo ameliambia mbunge kuwa Mzee Majuto ni msanii mkubwa sana na amefanya matangazo na kuingia mkataba na makampuni mengi sana mabyo yamekuwa yakirusha matangazo yake katika televisheni lakini mzee huyo hakufaidia  na kitu chochote.

Akiongea akiwa bungeni mh mwakyembe anasema kuwa “Mzee Majuto mwanasanaa mzuri anaumwa anaomba pesa, mimi leo nachanga kutoka mfukoni lakini leo hii nusu ya mabango ya biashara ni Mzee Majuto, matangazo ya biashara kwenye TV ni Mzee Majuto naomba sasa nitumie nafasi hii kusema nimeunda kamati ya wanasheria tumeanza na kesi ya Mzee Majuto mashirika yote na kampuni zote zilizoingia mkataba na Mzee Majuto tutapitia hiyo mikataba kama ameonewa lazima ilipwe familia yake tumeshachoka, tukimaliza Majuto tuna kuja mikataba ya Kanumba na msanii yoyote ambaye aliingia mkataba wa kipumbavu atuone”  .

download latest music    

Wasanii wengi wamekuwa wakiomba misaada pale wanapopata matatzo ilhali walikuwa na nguvu na jina kubwa ambalo lingeweza kuwaingizia pesa kwa kipindi chote cha ugonjwa au uzee kama Mzee Majuto.

Mzee majuto ameanza kuumwa tangu janauary mwaka huu na kufanyiwa upasuaji , ambapo hivi karibuni alirudishwa hospitali baada ya hai yake kuwa mbaya tena na kusemekana kuwa kidonda alichofanyiwa upasuaji kimeshindwa kufunga, mpaka sasa Mzee Majuto ameamishiwa hosptali ya muhimbili na wizara imepanga kumsaidia ili kupata hali zake za mikataba na matangazo mbalimbali aliyowahi kuyafanya.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.