“mimba ya wema haikuwa kiki”-Idris akiri

Ni muda mrefu umepita na kila moja amekuwa akiendelea na maisha yake ingawa wameonekana kuwa wapo karibu na kusapotiana kwa kiasi kikubwa katika biashara , lakini kwa bahati nzuri idris ameongea tena kuhusu yeye na  wema sepetu kwa mara nyingine tena.Idris sultan ambae alikuwa mshindi wa shindano la big brother africa na pia kwa sasa amejiingiza katika shughuli za biashara huku akiwa na lebel yake viatu vya kiume ameongea leo na kusimulia kwa undani kuhusu maisha yao kwa ujumla kipindi alipokuwa na mahusiano na Tanzanian sweetheart wema sepetu.

Akiongea na Dizzim online katika segment ya ‘chill and sky’ idris anasema kuwa ilikuwa ni kazi sana kwake kumsahau wema sepetu, kwa sababu katika mahusiano yao walipitia mengi sana hata hivyo idrisa anasema kuwa kwake wewe uwa anaangalia sana mambo mazuri aliyofanyiwa na watu kuliko vile vibaya ambavyo mtu hufanya.Idris anasema kuwa pamoja na sidechicks waliokuwepo lakini bado wema ni mwanamke aliyekuwa anampenda sana.

download latest music    

Idris ambae muda wote huonekana amejawa na utani mwingi, anasema kuwa hata ile issue ya kuwa wema sepetu kuwa mjamzito ni kweli akikuwa na mimba na wala haikuwa kiki kama vile watu walivyokuwa wanasema,’Sio kiki, ni kweli alikuwa na mimba..” na hata alipoulizwa kuhusu ukweli wa mimba iyo kuwa ni mapacha anasema ni kweli mimba iyo ilikuwa ni ya mapacha.

Pamoja na kuachana kwao lakini idris bado anaonekana kumpa heshima sana wema sepetu akisema kuwa alikuwa ni mwanamke wa kipekee tena anajua kabisa hakumpendea pesa zake na wema ni mtu ambae hakula pesa zake kabisa kama watu walivyokuwa wakiongea mitandaoni.

Akizungumziz mahusiano yake na mpenzi wake wa zamani kabla ya wema sepetu,Samantha ambae walikutana katika jumba la big brither,idris anasema samantha alikuwa ni mmoja wa watu ambao hakutaka kuongea nae kabisa kwa sababu alikuwa anajua sababu ya kuachana kwao ni wema sepetu lakini ukweli ni kwamba wema sio sababu,”..but we are good friends sasaivi..”idris aliongezea.

Akiongelea mahusiano yake ya sasa katika mapenzi ,idris anasema “niko very much single” huku akionekana kucheka.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.