Mimi Bado Ni Bikra – Jacqueline Wolper

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper ameibua mzozo mtandaoni baada ya kuandika na kudai kuwa yeye bado bikra.

Wolper amekuwa kwenye vichwa vya habari sana kwa mwaka huu wa 2017 aliuanza mwaka kwa kushangaza watu wengi na kuzua mjadala mzito baada ya kuweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na msanii kutoka WCB Harmonize lakini uhusiano wao pia uliisha kwa kishindo miezi michache iliyopita huku kila mmoja akimnyooshea mwenzake kidole kwa kujihusisha na usaliti.

download latest music    

Lamini Wolper hakuishia hapo alianza kutoka na kijana mdogo kwake au kwa lugha rahisi ni kiben-10 wake ambaye alijulikana kama Brown lakini nathubutu kusema uhusiano huuhaujawa mrahisi kwa Wolper kwani yeye na Brown wamekuwa watu wa kuachana na kurudiana na hivi sasa wameachana tena .

Wolper amezua gumzo tena kwenye mtandao wa kijamii baada ya kuanfika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa yeye ni msichana bikra ambapo aliandika “Wallahi I am still a virgin na mavirgin wenzangu tukutane High spirit kesho”. Hii ni kauli ambayo iliwashangaza wengi kwani inaelekea watu wengi hawakuamini kuwa Wolper anaweza kuwa bikra huku wengi wakidai kuwa amekuwa na uhusiano na wanaume wengi mpaka kuwa bado bikra.

Pamoja na hayo yote Wolper amesisitiza kuwa kwa sasa kitu pekee anachojali ni kufanya kaziJac zake na kukuza biashara zake ambapo duka lake la nguo la Wolper house of stylish linafanya vizuri sana

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.